Mfalme Mohammed VI wa Morocco akishuka kwenye ndege iliyomleta akiwa ameongozana na ujumbe wake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2016
Mfalme huyo amepokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli jioni hii, Mfalme Mohammed VI atakuwa nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Mfalme Mohammed VI wa Morocco akipokea shada la maua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA leo jioni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA jijini Dar es salaam jioni hii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akielekea karibu na ndege iliyomleta mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam.

Mfalme Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

Mfalme Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu huku akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Dk. Modestus Kipilimba kwa Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakati alipowasili jijini Dar es salaam leo.

Mfalme Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna John Casmir Minja huku akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akiongozana na Mwenyeji wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa JNIAleo jioni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi vya ngoma na Mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.

Mfalme Mohammed VI wa Morocco akipungia mkono wananchi waliojitokeza kumlaki huku akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

Ndege iliyomleta Mfalme Mohammed VI wa Morocco ikiwasili.

Ndege iliyomleta Mfalme Mohammed VI wa Morocco ikijiandaa kutua kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumlaki Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakati alipowasili jijini Dar es salaam .
No comments:
Post a Comment