• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 20 October 2016

    SERIKALI KUENDELEA NA MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA


    Na Masanja Mabula -Pemba .
    index 
    MKUU  wa Wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk Khatib amesema Serikali itaendelea na mpango wa mapambano ya matumizi ya madawa ya kulevya kwa kuwapatia dawa ya methadone vijana ambao wanatumia dawa ya aina ya heroin ili kuwalinda vijana wake ambao ni chanzo cha kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
     
    Amesema madawa ya kulevya  aina hiyo ni hatari kubwa kwa taifa na jamii kwani vijana wanaotumia wameathikara afya zao hali ambayo hulazimika kutumia fedha nyingi kuwapatia matibabu ili kurejesha hali zao.
     
    Salama ameyasema hayo katika  skuli ya Madungu sekondari wakati akifungua mafunzo ya kuwahamasisha viongozi wa wilaya za Pemba juu ya kupunguza utumiaji wa madawa ya kulevya unaopelekea maambukizo ya virusi vinavyosababisha ukimwi na homa ya ini.
     
    Amesema baadhi ya familia zimetetereka kutokana na vijana wao kuingia katika janga hilo la utumiaji wa dawa za kulevya na wameshindwa kuwatowa na hata kuwapatiwa matibabu kutokana na hali zao za kiuchumi katika harakati za kimaisha.

    “Madawa ya kulevya ni janga linalohatarisha maisha ya vijana na Taifa , kwani familia ambazo vijana wake wameathirika na  dawa za kulevya zimeshindwa kupiga hatua kimaendeleo na uchumi kutokana na kutumia fedha nyingi kuwatibu vijana hao “alisema.
     
    Nae Mratibu wa Kinga dhidi ya VVU na maradhi ya kujamiiyana kutoka kitengo shirikishi cha kifua kikuu , ukimwi na ukoma Zanzibar Shaaban Hassana Haji amesema athari ya madawa ya kulevya ya aina ya heroin imekuwa kubwa kwani vijana wanaotumia wamepata maambukizo ya Virusi vinavyosababisha ukimwi.
     
    Amesema hatua ya matumizi ya sindano moja kujidunga zaidi ya kijana mmoja siyo inaambukiza virusi vinavyosababisha ukimwi lakini inaambukiza homa ya ini aina ya ‘C’ ambayo matibabu yake yanahitaji kiasi cha shilingi milioni mia moja kwa kumtibu mgonjwa mmoja.

    “Matumizi ya dawa za kulevya aina ya heroin kwa kujidunga sio tu kwamba inaweza kusababisha maambukizi ya VVU pia inaweza kuambukiza homa ya ini aina ya ‘C’ ambayo matibabu yake ni zaidi ya shilingi milioni moja kwa mgonjwa mmoja “alifahamisha.
     
    Mafunzo hayo ya siku mbili na yanawashirikisha maafisa kutoja jeshi la Polisi, Makatibu Tawala wa Wilaya, wataalamu wa afya na maafisa kutoka Wanawake na Watoto na Wizara ya Elimu yameandaliwa na kitengo shirikishi cha kifua kikuu, ukimwi na ukoma Zanzibar kupitia Globa Fund.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI