• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 20 October 2016

    WANANCHI WALALAMIKIA KUFUNGWA KWA KITUO CHA POLISI NYAKATI ZA USIKU


    indexNa Masanja Mabula –Pemba

    WANANCHI wa shehia ya Kengeja wilaya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba  wamelililamikia jeshi la polisi  kituo cha Kengeja kukifunga kituo hicho nyakati za  usiku na baadhi ya askari kituoni hapo wakijishusisha na vitendo  vya ulevi hali ambayo inawapelekea kusumbuka pindi wanataka msaada kituoni hapo.
     
    Wamesema kuwa,tatizo hilo ni la muda mrefu sasa na kila siku hali inavyokwenda ndivyo hali inavyokuwa mbaya kituoni hapo.
     
    Hayo yameelezwa  na baadhi ya wanachi wa maeneo hayo kwa nyakati tofauti walipokua wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyefika kijijini huko kufuatia malalamiko juu ya kadhia hiyo.
     
    Mmoja miongoni mwa wanakijiji hicho ambae hakupenda jina lake liandikwe gazetini  amesema kuwa,hali ni mbaya katika kituo hicho na  inapofika majira ya saa nne usiku kituo  kinafungwa na hakuna huduma yoyoye inayopatikana kuzanzia wakati huo mpaka asubuhi.
     
    “Kwa kazi zangu, mara nyingi huwa narudi nyumbani usiku, nikipita kituo kimefungwa sasa najiuliza kama kumetokea  tatizo usiku huo kimbilio ni pale kituoni lakini kinafungwa ”alisema mkaazi huyo.
     
    Akizungumzia suala la ulevi kwa askari wa kituo hicho amesema kuwa, ni aibu kwa kituo hicho ingawa si wote lakini wapo baadhi yao hulewa mpaka muda wakazi.
     
    Amesema inafika wakati mtu anakwenda mapokezi kupeleka maelezo ya jambo fulani lakini anapigwa na mshangao kwa jinsi anaekupokea na kuandika shida yako akiwa hoi kwa ulevi.
     
    Sheha wa shehia hiyo Muhammed Kassim Afrika alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi juu ya kadhia hizo kwa askari wa kituo hicho amethibitisha na kukubali wazi uwepo wa askari walevi na kituo hicho kufungwa nyakati za usiku.
     
    Amesema kuanzia muda wa saa nne au saa sita usiku kituo hicho kinafungwa na baadhi ya wananchi hukosa humuda kituoni hapo.
     
    Sheha huyo ameungana na wananchi kwa kusema kuwa kadhia hiyo ni ya muda mrefu na ameshawahi kufikisha kilio hicho kwa kamanda wa Polisi Mkoa lakini mpaka leo hali bado haijarekebishika.
     
    Akigusia suala la askari wa kituo hicho kulewa wakati wa kazi amethibitisha madai hayo  huku akitilia mkazo sula hilo “ingawa sio wote lakini wapo baadhi yao wanalewa haswa tena kulewa”alisema sheha huyo.
     
    Kufuatia madai hayo ya wananchi yaliyotiliwa mkazo na sheha wa shehia hiyo mwandishi  wa habari hizi alikwenda mpaka katika afisi za kamanda mkoa wa kusini Pemba  Jeshi la polisi kituo cha Polisi Madungu na kuzungumza na kamanda huyo Sekhan Muhammed Shekhan.
     
    Akijibu suala la mwandishi wa habari aliyetaka kujua juu ya askari  wa kituo hicho kulewa Shekhan amesema,jambo hilo ameshalitolea taarifa kwa mwandishi wa habari wa awali aliyetaka kujua juu ya kadhia hiyo kuWa kuna matatizo kidogo katika maeneo ya kituo hicho.
     
    Amesema sio  askari wote wanaolewa  ila ni mmoja tu na hatua zimeshaanza kuchukuliwa kwa askari huyo.
     
    Akitaja hatua hizo walizozichukua dhidi ya askari huyo amesema,wamemuweka karibu na kamati zao za maadili ili kumchunguza zaidi na watakapomuona anaendelea na vitendo hivyo watamchukulia hatua za kinidham  ambapo tayari  wameshamuandikia barua ya tahadhari.
     
    Katika suala la kufungwa a kituo hicho nyakati za usiku amesema jambo hilo pia amelisikia na  bado wanaendelea kuchunguza kwa umakini  kwani sio suala la kuliharakisha.
     
     “Sisi tuna maafisa  mabalimbali amabao tumewapanga sehemu tofauti kwa kuchugunguza mambo kama hayo na baada ya kupata taarifa rasmi totatoa  jibu na ikibainika kinafungwa kweli tutamwita mkuu wa kituo kueleza ni sheria gani iliyompa kufunga kituo hicho  ambacho ni class “A”kwa sababu vituo kama hivyo havitakia kufungwa  ila vinatakiwa kutoa humuda muda wote” alisema Kamanda Shekhan.
     
    Amemalizia kwa kusema kuwa mpaka muda huu bado hawajawahi kuona kituo hicho kufungwa kwani wameweka askari wa wakufanya uchunguzi juu ya lalamiko hilo lakini bado hatajawahi kuona kufuli ilining’inia kwenye mlango wa kituo .

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI