• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 26 October 2016

    SHULE YA SEKONDARI MTAKUJA YAKABILIWA NA UHABA WA WALIMU

    Immaculate Ruzika
    SHULE ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi inakabiliwa na uhaba wa Mwalimu wa Hesabu, hali iliyosababisha, Diwani wa Kata hiyo Michael Urio kumlipa mshahara mwalimu wa somo hilo.
    Akizungumza jana katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi, Diwani wa kata ya Kunduchi ... alisema kuwa  shule hiyo ina uhitaji  mwalimu wa Hesabu wa kidato cha kwanza na cha pili.
    ''Nilivyoona kuna uhitaji wa mwalimu wa hesabu kidato cha kwanza na cha pili, niliamua kumtafuta mwalimu ambaye nitamlipa mshahara ili aweze kuwasaidia watoto hao'', alisema.
    Aidha Diwani huyo  alisema  wanafunzi hao wamekuwa katika mazingira kama hayo, tangu mwezi februali mwaka huu mpaka sasa, wala hakuna dalili za kupatikana mwalimu wa Serikali.
    Mkuu huyo wa Wilaya alimuahidi Diwani huyo, kuwa atawasiliana na Waziri wa TAMISEMI ili waangalie uwezekano wa kupata mwalimu wa somo hilo Shuleni hapo.
    Hapa alikuwa katika ziara ya kutembelea na kusikiliza kero za wananchi na kutatua matatizo yanayowakabili.
    mwisho

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI