• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 27 October 2016

    SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTANZIR YATOZWA FAINI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA


    Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati) alipofanya ziara ya kukagua mazingira katika kiwanda cha kutengeneza viroba vya mifuko Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam.     
    pina2
    Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (kushoto) mara baada ya kuwasili na kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Murzer kilichopo jijini Dar e s salaam.   
    pina4
    Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akikagua sehemu ya kuyeyushia viroba ya mifuko katika kiwanda cha Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam mapema hii leo.
    pina1
    Shule ya sekondari ya Almuntazir iliyopo upanga jijini Dae es salaam imetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kosa la uchafuzi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka ya chooni katika mto msimbazi ndani eneo la mikoko katika eneo la daraja la salenda na kujenga uzio wa ukuta bila kuzingatia mita sitini zinazotakiwa kisheria.
    Faini hiyo inatakiwa kulipwa ndani ya wiki moja imetokana na ziara ya Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina iliyofuatia malalamiko ya wakazi wa Upanga iliyompelekea Naibu Waziri kufanya ziara yakwenda kujionea uchafuzi huo.
    Akiongea kwa Niaba ya shule meneja wa shule hiyo Bw. Serialis Rwechungura amesema kuwa, watalipa faini hiyo kama ilivyoelekezwa na serikali na hakuwa tayari kuongelea swala la ukuta wa shule hiyo.
    Naibu Waziri Mpina amesisitiza kuwa serikali haitakuwa tayari kuwavumila wawekeajia wakiukaji wa sheria hasa ya mazingira, na kuweka rehani maisha ya watanzania.
    Aidha Naibu Waziri alitembelea maeneo  ya mwenge kijijini na kuonea uchafu wa mazingira uliotokana na kuvuja kwa maji taka ya choo kutoka kwenye miundombinu ya majitaka ya DAWASCO hali inayosababibsha wakazi na wafanyabiashara wa maeneo ya mwenge kushindwa kustahimili hali hiyo na kuwa hatarini kupata magonjwa ya maambukizi kama kipindupindu na homa ya matumbo.
    Akiikemea DAWASCO kwa mara nyingine kwa kutokuonyesha uwajibikaji na utii kwa mamlaka za juu, Naibu Waziri Mpina ameita NEMC kuiandikia DAWASCO faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kutelekeza miundombinu yao na kutakiwa kulipa adhabu hiyo kwa muda wa wiki mbili.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI