• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 27 October 2016

    WAIGIZAJI WA KIKE WAPIGWA MSASA KUONGEZA USHIRIKI WAO KWENYE TASNIA YA FILAMU NCHINI

    nl1
    nl1Afisa Mipango wa Bodi ya Filamu Tanzania Mfaume Said akiwasilisha mada inayohusu historia, majukumu na mipango ya baadae ya bodi hiyo mbele ya wasanii wa kike waliohudhuria mafunzo ya kuongeza ushiriki wao kwenye tasnia ya filamu. Mafunzo hayo ya siku mbili ni mwendelezo wa juhudi za Bodi ya Filamu kuongeza ubora wa filamu za Kitanzania.
    nl2
    Mkufunzi  kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Dkt. Mona Mwakalinga akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada inayohusu njia mbalimbali zinazotumika kuongeza uwezo wa mwigizaji kuuvaa uhusika kwenye michezo ya kuigiza na filamu.
    nl3
    Baadhi ya waigizaji wanaoshiriki mafunzo ya siku mbili ya kuwaongezea ushiriki waigizaji wa kike wakifuatilia mada inayowasilishwa na Mkufunzi Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Dkt. Mona Mwakalinga. Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika ukumbi wa Habari Maelezo, jijini Dar-es-salaam
    nl4
    Mwigizaji wa michezo ya kuigiza na filamu Bi. Madina Mjatta (Zawadi) akichangia mada wakati wa mafunzo ya siku mbili yanayolenga kuongeza ushiriki wa waigizaji wa kike kwenye tasnia ya filamu nchini.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI