• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 25 November 2016

    Baraza la Madiwani Lamfukuza Kazi Mtumishi




    Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Mji wa Bunda, mkoa wa Mara  Bi. Janeth Mayanja  akiwa Ofisini  kwake.

    Na. Immaculate Makilika 


    BARAZA la Madiwani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda limemfukuza  kazi  Bw. Eliud Haonga aliyekuwa mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango  na Mthamini  daraja la pili mapema wiki hii, baada ya kughushi nyaraka ili kujipatia fedha za malipo ya pango.

    Bw. Haonga alipokea fedha za malipo ya pango kiasi cha shilingi milioni saba kutoka kiwanda chaOLAM Tanzania mwezi Juni mwaka huu.


    Akizungumza kwa njia ya simu,  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mkoa wa Mara, Bi. Janeth Mayanja alisema kuwa Bw. Haonga amekiuka Sheria za Utumishi wa Umma, kanuni ya 42 na uamuzi uliotolewa na baraza la madiwani  ni sahihi.

    Bi. Janeth alisema “Bw. Eliud Haonga alihifadhi shilingi milioni mbili tu katika akaunti ya Halmashauri ya Mji wa Bunda  na kutumia shilingi milioni tano kwa matumizi yake binafsi”.

    “Maamuzi haya yamechukuliwa baada ya Kamati ya Uchunguzi  kumaliza kazi yake kwa mujibu wa  Sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.” alisema  Bi. Mayanja.

    Aidha,  Bi. Mayanja amewaasa watumishi wa Halmashauri  Bunda  kujiepusha na vitendo vinavyoashiria wizi na ubadhirifu,  na hatua kali  zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI