• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday 27 November 2016

    CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMETOA UFAFANUZI JUU YA MGOGORO UNAOENDELEA NDANI YA CHAMA HICHO

    NEEMA HUSSEIN
    Chama cha wananchi CUF kupitia katibu mkuu wa chama Maalim Seif Sharifu Hamadi ameitisha mkutano na waandishi wa habari ili kuanisha kasoro mbalimbali ambazo hufanywa na baadhi ya wanachama pamoja serikali.

    Maalim Seif amewatupiwa lawama Profesa Ibrahimu Lipumba pamoja na msajili wa vyama vya siasa nchini jaji Francis Mutungi kwa kutumia nguvu ya kumtambua Lipumba kama mwanachama halali na Mwenyekiti wa CUF.

    Hali yakuwa wajumbe 46 kati ya 53 walimtaka Lipumba avuliwe uanachama pamoja na uenyekiti.

    Katika hatua nyingine na kuelekeza mgogoro baina ya chama hicho na jeshi la polisi Maalim Seifu amesema jeshi la polisi limekaa kimya dhidi ya vitendo vya jeshi hilo kukataa baadhi ya mikutano. Lakini pia akizungunzia  mkutano wa blue peal ambao ulisababisha uharibifu mkubwa ambao thamani ya vilivyo haribika ni zaidi ya milioni nane na mkutano huo uligharimu milioni mia sita.
    \
    Pili utekwaji wa baadhi ya viongozi akitolea mfano Joran Bashange ambapo inadaiwa Lipumba anahusika katika njama hizo. Pia kuzuiya kufanyika kwa baadhi ya mikutano ametolea mfano Mtwara na Lindi licha ya kutuma barua yenye walaka CUF/HQ/AKM/003/016/032.  Pamoja na kuzuiya mkutano huko Tanga. Akiongeza kuhusu Lipumba kuwa alijiudhuru mwenyewe Agusti 06 mwaka huu wakiwemo viongozi wote wa chama hicho wakimsihi asijiudhuru

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI