• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday 27 November 2016

    MKUU WA MKOA MAKONDA AWAPA ONYO WENYEVITI DAR

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya DARMPYA ambapo siku ya leo ni zamu ya wilaya ya Kinondoni.rc-makonda-kino-5rc-makonda-kino-5

    Akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni RC Makonda ametoa agizo kwa Wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wamekuwa wanaitumia kinyume na utaratibu kwa kudhulumu haki za wanyonge ikiwemo kuuza viwanja kinyume na utaratibu, huku akisisitiza kuwa watendaji wa mtaa ndiyo inabidi wakae na mihuri hiyo.rc-makonda-kino-4

    Pia RC Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum cha kisheria kitakacho Tamika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na kuwashauri wananchi kabla ya kuipeleka mahakamani na kuwaweka wazi kama kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa suluhisho la kudumu.rc-makonda-kino-3

    Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa Kinondoni Bernard Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na kuhakikisha vinatoka kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.rc-makonda-kino-2

    Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi kuwashughukia watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili kuchochea maendeleo.

    Jiunge nasi 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI