• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 10 November 2016

    MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AONGOZA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA MAPOKEZI YA MWILI WA SPIKA MSTAAFU MHE. SAMUEL SITTA

     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea mjane wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta, Mama Margaret Sitta (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
    Jeneza lenye mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta likiwa limebebwa na askari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaongoza viongozi mbali mbali wakati wa mapokezi ya mwili wa  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta
     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
    Hassan pamoja na  Katibu Mkuu wa UWT Mhe. Amina Makilagi (kushoto) wakimfariji akimfariji Mama
    Margaret Sitta (katikati) wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
    wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta kwenye uwanja wa ndege
    wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza viongozi na
    wananchi  katika mapokezi ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
    Nyerere Jijini  Dar es Salaam ukitokea nchini Ujerumani alipofariki wakati anapatiwa matibabu.
     
    Akizungumzia jinsi anavyomfahamu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
    Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Taifa limeondokewa  kiongozi mwadilifu,mzalendo, mchapakazi na mtetezi
    wa wanyonge hivyo taifa litaendelea kuumuenzi
    utendaji wake.
    Viongozi mbalimbali waliojumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
    Samia Suluhu Hassan katika mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu Samweli Sitta
    kweye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere ni pamoja na Makamu wa
    Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Seif Ali Iddi, Waziri wa Mambo ya
    Nje, Ushirikiano wa Afrika, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga  na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
    Baada ya
    Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta kuwasili nchini leo mchana amepelekwa
    nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam ambapo hapo kesho asubuhi viongozi
    na wananchi watatoa heshima zao ya mwisho za kuuaga mwili wa marehemu katika
    viwanja wa Karimjee jijini

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI