MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda, amepiga marufuku wauzaji holela wa samaki na mbogamboga mitaani na kuagiza jeshi la polisi na halmshari zote mkoani humo kuwakamata wafanyabishara watakao kikuka agizo hilo.
Makonda ametangaza hatua hiyo , jana, wakati alipotembelea Soko la Kimataifa la Samaki (Feri) na kuzungumza na wafanyabiashara katika soko hilo ambao walieleza kuwa, moja ya changamoto zinazo wakabili ni pamoja na kuzagaa kwa wafanyabiashara huria wa samaki hususan katika vituo vya mabasi ya daladala na bararani mkoani humo.
Wafanyabiashara hao, walidai kuwa, hali hiyo inahatarisha uhai wa soko hilo kwani watu wengi hawafiki kununua samaki katika soko hulo, badala yake huishia kununua katika vituo vya mabasi na mitaani.
Mfanyabiashara Said Ally ‘Ngasa’ alimueleza mkuu huyo waa mkoa kuwa, masoko huria ya mitaani yanasendelea kushamiri huku viongozi wa halmshauri na wananchi wakikaa kimya.
“Hivi sasa kila kona kuna watu wanauza samaki hasa katika vituo vya mabasi. Hapa feri tunakosa wateja. Wanaishia hukohuko mtaani. Hili soko litakufa kwa sababu watu hawaji tena tofauti na awali,”alisema Ngasa.
Aliongeza;“Naomba wafanyabishara katika vituo vya mabasi washughulikiwe. Hapa soko linakufa. Biashara imepotea,”
Mohamed Nasoro ambaye ni muuzaji wa mbogamboga katika soko hilo, alisema uuzwajji holela wa mbogamboga mitaani unaua soko la bidhaa hiyo, hivyo kumuomba mkuu huyo wa mkoa kuchukua hatua dhidi ya wafanyabiashara waliozagaa mitaani.
Mbali na hayo wafanyabiashara hao waliomba kuboreshwa kwa miundombinu ya soko hilo ambayo imechakaa licha ya soko kuwa la kimtaifa.
Kufuatia kilio hicho, Makonda alichua uamuzi wa kupiga marufuku biashara ya samaki na mbogamboga mitaani na kumuagiza Kamanda wa Operesheni , Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya kuwashughulikia wafanyabiashara wote watakao kiuka agizo hilo kuanzia leo.
No comments:
Post a Comment