Habari
NA AHMED KOMBO
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Bakari Shingo Gongo la Mboto wakimtuhumu kufoji risiti pai hutumia lugha chafu kwa wananchi wake kipindi wanapo kwenda kutatua matatizo madogo madogo na hupenda kufanya vikao usiku
Lawama hizo zimempelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye yupo kwenye ziara yake katika wilaya ya Ilala Pugu Kajiungeni, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Salum Hamduni kumsweka rumande Mweyekiti huyo mpaka upelelezi utakapo kamilika.

- IF
Akitoa ushahidi kuhusu sakata hilo Mkazi wa Gongo la Mboto na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pili Seif ameeleza kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa zimefikishwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Jiunge
No comments:
Post a Comment