• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 23 November 2016

    KAMISHENI YA UTALII YATAKIWA KUTAFSIRI VITABU VYA UTALII

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Kamisheni ya Utalii Zanzibar italazimika kutafsiri vitabu vya utalii kwa lugha mbalimbali za kimataifa ili kuutangaza vizuri utalii Visiwani Zanzibar ili kwenda sambamba na kasi ya serikali ya kuimarisha miundombinu katika Sekta ya Utalii.

    Amesema wakati umefika kwa kamisheni hiyo kufungua njia zaidi za kuutangaza utalii wa Zanzibar kwa kuhamasisha watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani zikiwemo nchi za Ghuba badala ya kuelekeza nguvu kubwa kwa mataifa ya Ulaya na Amerika.BALOZI SEIF

    Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo wakati akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhandisi ya Naif Khadija Naif Alyafei aliyejitolea kuwa Balozi wa kuitangaza Tanzania kwenye fursa za biashara na masuala ya utalii katika Mataifa ya Ghuba akilenga zaidi Nchi ya Saudi Arabia, mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar na kusema mataifa mengi ya Ghuba yanaonesha kwamba wananchi wake wanapendelea utamaduni wa Tanzania lakini wanashindwa kuuelewa kwa kina kutokana na vitabu vingi vya Kamisheni ya Utalii Zanzibar kuandikwa kwa lugha chache kama za Kingereza na Kifaransa.

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kwa vile jamii ya dunia imetawaliwa na lugha tofauti, kamisheni hiyo ijikite kutekeleza jukumu hilo muhimu  na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo itawajibika kugharamia kazi hiyo.BALOZI SEID

    Mapema Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhandisi ya Naif Khadija Naif Alyafei amesema taasisi yake imejikita zaidi katika kuwahamasisha wajasiriamali wadogo wadogo ili wapate nafasi ya kuzitangaza biadhaa wanazozalisha katika fursa za kibiashara zilizopo katika Mataifa ya Ghuba

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI