• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 23 November 2016

    RC MAKONDA KUFANYA HAYA KWA WATUMISHI WALIOKAA MUDA MREFU

    Katika Muendelezo wa ziara yake ya kuitafuta DARMPYA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo yupo Wilaya ya Ilala baada ya kuhitimisha ziara yake siku ya jana leo katika Wilaya ya Temeke.rc-makonda-ziara-ilala-16

    Akizungumza na watumishi wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya Ilala katika ukumbi wa Anatoglo RC Makonda amesisitiza kuhusu uwajibikaji na kueleza kuwa hawataki watumishi mizigo katika Mkoa wake huku akisema kuwa hatawahamisha mkoa watumishi ambao wanamuda mrefu na hawajatimiza majukumu yao ipasavyo.

    RC Makonda amesema kuwa kufanyakazi kwa muda mredu inabidi kuendane na uwajibikaji bora wenye manufaa kwa wananchi, pia RC Makonda amesemna kuwa wale watumishi waliopata nafasi za ajira kupitia watu fulani wajiandae kwani amejipanga kuwawajibisha kama wasipo wajibika.rc-makonda-ziara-ilala-11

    Kwa upande wake Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa ya  Ilala Edward Mpogolo anaemuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema, amemuomba RC Makonda kuipa Ilala kipaumbele kwa kuongeza vituo vya Afya, na kumtaka awaongezee vituo vya polisi kama ulivyo mpango wake wa kuongeza vituo 20 kwa Mkoa wa Dar es Salaam

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI