
Baada ya kufanyika mashindano ya Miss Tanzania 2016, moja ya wadhamini waliojitolea kutoa sapoti mwaka huu, Kampuni ya Teknolojia ya Magari (PII) imeingia mkataba wa mwaka mmoja na mshiriki wa mashindano hayo na pia ni Miss Kilimanjaro 2016, Glory Stephen Minja kuwa balozi wa kampuni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo, Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Teknolojia ya Magari (PII), Ebenezer Msuya, amesema kuwa kampuni yao imeingia mkataba na Minja kutokana na uwezo ambao ameonyesha kwa kipindi ambacho walikuwa wakidhamini mashindano ya Miss Tanzania na baada ya kuchambua uwezo wa kila mshiriki na kuona kuwa Glory anauwezo mkubwa hivyo wanaamini kuwa watafanya naye kazi vizuri.
Aidha alisema kuwa walikuwa wanaangalia uwezo pamoja na kuwapa bussiness card na tukataka ziwe na mrejesho, tukawapa na diary na pia tulikuwa na jaji ambaye aliwaangalia kwa siku nne na sisi tunataka mtu ambaye atakuwa tayari kufanya kazi za kijamii na kibiashara hivyo ataweza kupeperusha bendera yetu
“Mpaka sasa tayari ametuletea mawasiliano ambayo yana tija, amekuwa balozi wa PII na sisi tutashirikiana nae kufanikisha mikakati yake na sisi atatusaidia kufanikisha biashara yetu, kuna mawazo ambayo amekuja nayo na hatukuwa nayo mwanzoni tunataraji tutafanya nae kazi vizuri,” alisema Msuya.
Kwa upande wa Miss Kilimanjaro 2016, Glory Minja amesema ni nafasi ya kipekee kufanya kazi na kampuni hiyo ambayo imejikita zaidi katika teknolojia na atatumia nafasi aliyonayo katika jamii kuhakikisha anafanikisha malengo ambayo wanataka kuyafikia.
“Nawashuru familia ya PII kwa kunikubali na kuwa balozi wa kampuni yao, walianza kudhamini mashindano ya Miss Tanzania na nimejifunza mengi kutoka kwao kwa hicho kipindi na matarajio yangu ni kufanya nao kazi vizuri sana na sitawaangusha”alisema Minja.
Hata hivyo pamoja na kampuni ya PII kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Glory pia imemkabidhi hundi ya milioni moja ikiwa ni sehemu ya ahadi ambayo PII ilitoa kwa washiriki wa Miss Tanzania 2016 kuwa atakayechaguliwa kuwa balozi atapatiwa kiasi hicho cha fedha ambazo zitamsaidia kusaidia kijamii hasa katika mkoa wake.
No comments:
Post a Comment