MKURUGENZI na Mbunifu wa kampuni ya Star Natural
Products George Buchafwe amewataka
watanzania kumuunga mkono Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli katika
kutekeleza kauli yake ya Tanzania viwanda pamoja na kuwa wabunifu,wazalishaji na
kulipa kodi
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana
wakati maonyesho ya kibiashara yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee
alisema kuwa nchi yoyote haiwezi kuendelea pasipo kuwekeza katika viwanda
vidogo vidogo.
Alisema kuwa kampuni yake imewekeza katika kutengeneza
sabuni na mafuta yaliyotengenezwa na mawese na imeajiri watu Zaidi ya 25, na
kuwashauri vijana wasikae mtaani kusubiri kuajiliwa badala yake
wajishughulishe.
Aliongeza kuwa kiwanda chake kipo chini ya SIDO na kina dhamana
pana ya kukuza viwanda vidogo,kutoa mafunzo na kuendeleza mawazo kwa
wajasiliamali wapya wanaotaka kujiunga na uzalishaji wa kuchakata mafuta ya
mawese na uzalishaji wa sabuni bora.
“Katika uzalishaji tumebuni mashine nzuri kwa ajili ya
uzalishaji wa mafuta na sabuni katika kuzingatia lengo kuu la millennia ya
kupiga vita umaskini, na kuumunga mkono Rais Magufuli na nchi yoyote haiwezi
kuendeloea pasipo watu wake kujishughulisha”. Alisema George
Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Mic Global Risks Scholastica
Mtey alisema kuwa lengo la maonyesho hayo ni kutoa fursa kwa watanzania
kujifunza kuwa kampuni yake inatoa bima ya afya inayowezesha kutibiwa nchi
aipendayo
Alisema kuwa mtu akijiunga na huduma hiyo anapata uhuru wa
kuchagua nchi au Taifa alitakalo na kampuni hiyo itasimamia huduma zote za
matibabu , nauli na gharama zote atakazozitumia na kuwataka watanzania kujiunga
kwa wingi na mfuko huo
No comments:
Post a Comment