Serikali imewataka wahitimu wa chuo cha biashara CBE kampasi ya Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanatumia fursa zilizopo
ndani ya nchi na nje ya inchi ilikujiletea maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa nan a waziri wa viwanda viwanda
biashara na uwekezaji mheshimiwa charse mwijage akizungumza na wahitimu wa chuo
cha biashra CBE kampasi ya Dar es salaam walio hudhuria maafali ya 51 chuoni
hapo jijini dar es salaam.
Amesema serikali imeendelea kudumisha ushirikiano na nchi za
jirani kupitia jumuiya ya afrika mashariki EAC,na jumuia ya maendeleo ya nchi
za kusini mwa afrika SADC,tumekubaliana
kuondoa vikwazo mbalimbali vya kiuchumi, kijamii, na biashara katika nchi
zilizo kwenye ukanda huu ilikuwezesha wananchi kunufaika Zaidi nafursa zilizopo
nje ya nchi.
Hata hivyo alisisitiza pamoja na changamoto zilizopo kwa
watanzania lakini jambo la umuhimu ni
kuamua na kudhubutu kwa hivyo tutumie fursa hii kuwaimiza wahitimu waombe kazi
hata zilizopo nje ya Tanzania.
Aidha mkuu wa chuo cha CBE Prof Emanuel Mjema alisema kuwa kutukana
naongezeko la mahitaji ya taaluma chuo cha elimu ya biashara kimelazimika
kuongeza udahili wa wanachuo wakati miundominu yake bado ni ile ile ya zamani
ambayo imekifanya chuo kutoa elimu katika mazingira magumu katika kampasi yetu
ya Da es salaam,miundombimu iliyopo iliwekwa ihudumie wanachuo 600 tu na sasa
inahudumia wanachuo Zaidi ya 6000, kwa sasa tuna uhaba mkubwa za mihadhara,
maktaba ya kisasa na ofisi ya wanafunzi.
No comments:
Post a Comment