• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 29 November 2016

    WAZIRI MWIJAGE: WATANZANIA ASILIMIA 40 WANATAKIWA WAWE KATIKA UCHUMI WA VIWANDA IFIKAPO 2020

    Watanzania takribani asilimia 40 wanatakiwa wawe wamejiingiza kwenye uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020 ili kuweza kusaidia kukuza ajira za vijana na kuifanya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla. waziri-mwijage
    Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage amesema kuwa Serikali imeazimia kufikisha asilimia 40 ya watanzania kufanya shughuli za uchumi wa viwanda kufikia 2020.

    “Tunataka mpaka kufikia 2020 watanzania takribani asilimia 40 wawe wamejikita kwenye uchumi wa viwanda ili kusaidia kukuza ajira kwa vijana na kuifanya Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii nan chi yetu kwa ujumla” alisema Waziri Mwijage.mwijage-na-gsi

    Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa Uchumi wa viwanda unatakiwa kukua nchini kuwezesha kuzalisha bidhaa bora zitakazouzwa ndani na nje ya nchi ili kukusanya kodi kwa ajili ya kupata huduma bora za kijamii kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania .

    Jiunge nasi 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI