• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 29 November 2016

    JAMII IMETAKIWA KUWAHUSISHA WANASHERIA ILI KUEPUSHA MIGOGORO

    gamaya-tlsMigogoro mingi ya Kisheria katika masuala ya Ardhi, Ulipaji Kodi, Biashara, Ajira, Mirathi na Ndoa kwa Asilimia 80 inachangiwa na ukosefu wa Elimu juu ya masuala ya kisheria na kitendo cha wananchi kutowausisha wanasheria kabla ya makubaliano.gamaya-tls

    Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara (TLS) Kaleb Gamaya amesema ni muhimu kwa kila mwananchi kutambua kuwa kutafuta suluhisho katika ofisi za watendaji na kwa viongozi wa kisiasa si suluhisho la changamoto zao bali wajenge tabia ya kuwashirikisha wanasheria kabla ya kuingia makubalianao yoyote.

    Mwenyekiti  Kamati ya msaada wa kisheria kutoka chama hicho Maria Matui amesema msaada wa kisheria ni haki za Binadamu na kwamba ili maendeleo endelevu yafikiwe kikamilifu ni wajibu wa serikali na jamii kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanafuata sheria ili kutowanyima haki watu wengine.

    Wakiongelea muswada wa sheria ya msaada wa kisheria ambao unajadiliwa hivi sasa, wameiomba serikali kupunguza masharti kwa wasaidizi wa kisheria hasa katika kipengele kisicho mtaka msaidizi kutojihusisha na siasa kwani kuna wanasheria wengine ambao ni wabunge hivyo kipengele hicho kinaleta mkanganyiko juu ya utekelezaji wake.

    Jiunge nasi 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI