• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 20 November 2016

    ZIARA YA DC MAKONDA YAIBUA MAPYA KIGAMBONI

    Mkuu wa wilaya ya  kigamboni Hashim Mgandilwa ameitaka  Serikali  kuangalia upya juu ya malipo ya magari ya watumishi wa serikali wakati wa kuvuka daraja la kigamboni  jijini Dar es Salaam.img_9836

    Hata hivyo  Shirika la Hifadhi ya Jamii [NSSF] linapaswa  kuangalia upya malipo hayo yanayo fanyika kwenye daraja la kigamboni.asilimia kubwa ya watumishi wa umma wanaoishi nje ya Halmshauri hiyo kutozwa fedha kuvuimg_9874ka katika daraja hilo jambo ambalo linaleta changamoto kwa watumishi hao

    “Magari ya Halmashari yanayopita hapa daraja lininatozwa kiasi cha fedha shilingi 2000,hasa ikizingatiwa kuwa halmashauri hii ni mpya lakini asilimia kubwa ya  watumishi wengi wanatokea nje ya halmashauri hii,”alisema.img_9851

    Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la malipo  yanayo lipya kwenye daraja hilo,   alikubali kupokea malalamiko na kutaka kupunguziwa au kuondolewa bei hiyo 

    “tumekuwa tukipokea malalamiko hayao kutoka kwa wananchi wengi kuhusu suala hilo ni kwamba sisi kama huwa hatupangi gharama za malipo ya kuvuka daraja hili ila tunapokea maelekezo kutoka juu (Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi),”alisema.


    img_9874

    Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Makonda alimesema chanzo cha magari ya Halmashauri hiyo kutozwa tozo ni kutokana na mchakato na ujenzi wa daraja hilo kufanyika kabla ya Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni kuanzishwa.img_9874

    Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya kigamoni  Hashim alitumia nafasi hiyo kumuomba RC Makonda  kuunganisha barabara ya vumbi katika eneo la Vijibweni kwenda darajani urefu wenye  kilometa 1.5 ili kuondoa kuondoa  kero kwa wananchi wanoishi eneo hilo na wanaotumia barabara hiyo.

    “Barabara hii licha ya kutumiwa na watu magari baiskeli na pikipiki zinazopita darajani, ijapokua haijajengwa kwa kiwango cha lami nina imani wananchi wangu mnapata kero kubwa kutokana na ubovu na vumbi unao tokana na barabara hii nina waomba muwe na  uvumilivu  wenu wa muda mchache  ,”alisema Mgandilwa.img_9906

    Akihutubia wananchi wanaoishi karibu na mradi wa daraja hilo,RC Makonda amewahikishia kuwa barabara hiyo itaanza kujengwa baada ya wiki mbili ili kuondoa changamoto wanazokutana nazo wananchi

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI