Habari
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange kufutia kifo cha Bregedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki, Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar.

Katika salamu hizo za rambi rambi, Dk. Shein ameeleza kuwa amepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Bregedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki, Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar, kilichotokea jana katika Hospitali ya Jeshi la Wananachi wa Tanzania, Lugagalo, Dar-es-Salaam.
Dk. Shein kwa niaba yake pamoja na wananchi wote wa Zanzibar, ameeleza kuwa wamepokea kwa mshtuko, taarifa ya kifo cha kamanda huyo hodari aliyetoa mchango mkubwa katika shughuli za ulinzi na usalama na maendeleo ya nchi.
Aidha, salamu hizo za rambirambi zilieleza kuwa Marehemu Mhaiki ameacha pengo kubwa kwa familia yake, Brigedi ya Nyuki, Jeshi la Wananachi wa Tanzania pamoja na nchi nzima kwa jumla huku akisisitiza kuwa mchango wake hautasahaulika.
Dk. Shein amemuomba Jenerali Mwamunyange kuzifikisha salamu hizo za rambirambi kwa Wanafamilia, Maofisa na Wapiganaji wa vikosi vyote vya Ulinzi na Usalama sambamba na kuwaombea wafiwa wote kwa Mwenyezi Mungu awape moyo wa
subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Jiunge nasi
No comments:
Post a Comment