..

Thursday, 15 December 2016
Habari
Serikali imezindua ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria ya mwaka 2015/16 mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni awamu ya tatu katika ugonjwa wa malaria ambapo ripoti imeonesha kupungua kwa vifo vya watoto wadogo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mgeni Rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuaanda ripoti iliyoonesha Taifa kupiga hatua katika utoaji wa huduma ya mama na mtoto.
“Ripoti hii imeonesha kuwa bado kuna changamoto katika mimba za utotoni kwani zimeongezeka ukilinganisha na mwaka 2010 ambapo watoto 23 kati ya mia moja walipata mimba wakiwa na umri mdogo ukilinganisha na sasa watoto 27 kati ya mia moja hupata mimba katika umri mdogo hivyo kuna haja ya jamii kuelimishwa juu ya madhara ya mimba za utotoni”, alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa amesema kuwa iwapo huduma za afya zitaboreshwa zitapelekea ukuaji wa uchumi kwasababu ya uwepo wa nguvu kazi ya uhakika na kuongeza uzalishaji kwa Taifa.
No comments:
Post a Comment