• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 15 December 2016

    WAZIRI MPANGO MGENI RASMI MAHAFALI YA TISA CHUO CHA KODI DESEMBA 17

    Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango anatarajia kuwa mgeni rasmi  katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kodi yanayotarajiwa kufanyika  Desemba 17,2016 katika Ukumbi wa Mwl.J.K Nyerere Convection Centre  Jijini Dar es Salaam.

    ita
    Katika Mahafali hayo jumla ya wahitimu 558 watatunukiwa vyeti,shahada na stashahada ambapo kati yao wahitimu wa  kike ni 201 na wa kiume 357.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari  Mkuu wa Chuo hicho, Prof.Isaya Jairo amesema kwa mara ya kwanza tangu  kuzinduliwa kwa mitaala ya Astashahada ya Uzamili na Stashahada ya Uzamili katika Uongozi wa Forodha ya Afrika Mashariki,chuo kitatunuku  Astashahada ya Uzamili ya Uongozi wa Forodha ya Afrika Mashariki (Post  Graduate Certificate in Customs Administration (PGCCA).

    Prof.Jairo amesema Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunuku Cheti hiko.Amesema Jumla ya  Wahitimu 77 watatunukiwa PGCCA wote kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA).mpango

    Pia amesema kuwa Chuo kinashirikiana na Mamlaka za Mapato  za nchi wanachama wa Afrika Mashariki pamoja na zile za Ukanda wa Maendeleo wa Nchi as Kusini mwa Afrika (SADC) kama vile Botswana, Swaziland, Namibia, Zambia, Afrika Kusini, Zimbambwe na Malawi katika kuwajengea uwezo Wafanyakazi wa Taasisi hizo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI