Na Ahmed kombo Z4news blog
Ukuaji wa uchumi nchini unaonyesha unaendelea kukua kwa kiasi kubwa zaidi kulinganisha na mataifa mengine na kuwa miongoni mwa Nchi za bara la Afrika , Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakuwa ikifuatiwa na Congo DRC na Rwanda,Kenya, Uganda, Burundi, Afrika ya Kusini, Zambia na Malawi.
Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango amesema kuwa kukua kwa uchumi kunapimwa kwa kuangalia shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ni pamoja na uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na uvuvi, uzalishaji wa bidhaa za viwandani na migodini, ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali za kwa jamii ikiwemo afya, elimu na maji.
"Kasi ya kuongezeka au kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi ni mojawapo ya vitu vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa Taifa kwa ujumla ambapo kiashiria kimojawapo kinachotumika kupima ukuaji wa uchumi ni ukuaji wa pato la Taifa."
Aidha Dkt Mpango ameongeza kuwa kiashiria kingine ni mfumuko wa bei bao unapima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya ambapo ulipungua kutoka asilimia 6.5 januari 2016 hadi asilimia5.5 juni na kupungua zaidi hadi kufikia asilimia 4.5 na kupanda hadi asilimia 4.8 mwezi novemba 2016.
Amesema katika mwezi huo wa Novemba takribani nchi zote zilikuwa na ongezeko la mfumuko wa bei kutokana na kuyumba kwa ugavi wa chakula katika nchi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupanda kwa bei kwa bei za mafuta katika soko la Dunia.
Dkt Mpango amesema kwa tathimi ya upande wa mabenki unaonyesha kuwa benki yanaendelea kuimarika huku yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha kwa kuangalia uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi ambao ulikuwa kwa asilimia 37.46 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20.
" amana za wateja katika benki zilipungua kidogo kutoka Trilioni 20.73 mwezi Desemba 2015 kufikia shilingi Triliani 20.57 mwezi septemba kutokana na uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika ya Umma kutoka benki ya biashara kwenda benki kuu ya Tanzania."
Hata hivyo Mpango amesema kwa kuzingatia mwenendo wa ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha Januari hadi septemba 2016 matarajio ni kwamba kasi ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2016 na 2017 unatarajiwa kufikia hadi asilimia 7.2 kama ilivyokaririwa awali.
No comments:
Post a Comment