• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 30 December 2016

    MKUU WA WILAYA YA ILALA AGIZA MAZITO KWA MKURUGEZI WA ILALA

    Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Msongela Nitu na Mstahiki Meya Charles Kuyeko kusimamia kikamilifu Mradi wa DMDP uliosainiwa leo kati ya Halmashauri hiyo na China Railway Seventh Group, ambapo kwa awamu ya kwanza utahusisha ujenzi wa miundombinu ya daraja na barabara.

    dc-mjema-dmdp-10

    DC Mjema amefafanua kuwa mradi huo wa DMDP utapendezesha mitaa na kuondoa foleni jambo ambalo litawasaidia wananchi wa maeneo husika hivyo ametaka Mkurugenzi na Mstahiki Meya kuhakikisha kuwa barabara na Madaraja yanaisha kwa wakati kama ilivyopangwa ni kwa mwaka mmoja  na yawe ya viwango vya hali ya juu na zisiwe za kurudiarudia.dc-mjema-dmdp-9

    DC Mjema ameeleza kuwa mradi huo utazipitia barabara za Ndanda, Olympio, Kiungani, Omary Londo na Mbarouk ambazo zote zitakuwa na urefu wa kilomita 2.8 kwa kila moja, ambapo katika hatua nyingine DC Mjema amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha maroli yaliyozidi kiwango cha kubeba mizigo hayapiti kwenye miundombinu hiyo kwani yataleta uharibifu.dc-mjema-dmdp-15

    Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Charles Kuyeko ameeleza kuwa watajitahidi kuusimamia kikamilifu mradi huo wa DMDP ambapo zaidi ya bilioni 11.1 zimetengwa na Benki ya Dunia kwa ajili ya Mradi huo, huku Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Msongela Nitu akihaidi kuyafanyia kazi maagizo yote ya Mkuu wa Wilaya.dc-mjema-dmdp-6dc-mjema-dmdp-3

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI