Jeshi la polisi nchini kupitia kwa msemaji wake mratibu mwandamizi Advera Bulimba limetoa onyo kwa wananchi waliojipanga kufanya uhalifu katika kipindi cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Akiongea na waandashi Dar es salaam mratibu mwandamizi Advera Bulimba amesema…>>>’Tunaelekea
katika kipindi cha mwisho wa mwaka ambapo kuna sikukuu za kufululiza
lakini katika uzoefu tumeona ni muda ambao baadhi ya watu wamekuwa
wakitumia fursa zilizopo‘
‘Lakini
pia wapo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia nafasi hizo kwa ajili ya
kufanya uhalifu ikiwa ni pamoja na wale wanaojipatia kipato kisicho
halali‘ –Advera Bulimba
‘Jeshi
la polisi tumejipanga vyema na hatutaruhusu mtu yeyote aharibu amani ya
nchi kwa sababu zake binafsi, tunaomba wananchi watoe ushirikiano wa
kutosha katika kushiriki ulinzi shirikishi‘ –Advera Bulimba
No comments:
Post a Comment