• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 14 December 2016

    MAAMBO YAANZA KUFUKUTA KOMBE LA MAPINDUZI


    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    CHAMA  cha Soka Zanzibar (ZFA) kimetaja Kamati ya kusimamia mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) ambayo  imezinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na MichezoOmar Hassan Omar ‘King’..
    Mashindano ya Mapinduzi Cup yatakayoshirikisha timu tisa kutoka Uganda, Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar yatafanyika katika uwanja wa Amani kuanzia  tarehe 30 mwezi huu.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi ni Sharifa Khamis na Katibu wa Kamati hiyo ni Khamis Abdalla Said.
    Wajumbe wa Kamati ni Ali Khalil Mirza, Khamis Mzee Ali, Juma Mmanga, Ravia Idarous Faina, Mohammed Ali, Mohammed Ali Hilal, Issa Mlingoti Ali, Dk. Ally Saleh Mwinyikai na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Omar Hassan Omar ‘King’.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI