Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa. Harambee hiyo ilifanyika sambamba na mkutano wa hadhara uliohutubia wa Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa katika mkutano wa hadahara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Topa (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwam Issa Njinjo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment