Mke wa beki wa Simba, Juuko Murshid amejifungua watoto watatu.
Mkewe
aitwaye Ruth amejifungua watoto watatu usiku wa kuamkia leo wakati beki
huyo akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ amesema nao wamepokea taarifa hizo njema.
“Kweli tumepewa taarifa hizo ambazo ni njema, kwamba amejifungua watoto watatu mapacha,” alisema Abbas.
Beki huyo hajajiunga na Simba katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa yuko kambini na kikosi cha The Cranes.
No comments:
Post a Comment