Kauli hiyo ameitoa mapema hii leo katika ukumbi wa Karimjee jiijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kero zinzodaiwa kufanywa na mawakala hao wakiwa katika majukumu yao .
''Wakala anatakiwa kuvaa sare na sambamba nakitabulisho cha kazi ,sambamba nahili wakala anatakiwa kuwa namashine za EletronicFiscaldevice (Efd )ambazo zinatoa risiti zenye muhuri wa Manispaa''Alisema Meya Isaya Mwita .
Mwita alisema kuwa atafanya ukaguzi juu ya utekelezaji wa maagizo hayo ifikapo january Mosi mwakani nakuwataka wananchi kuwa makini kwawatu ambao wanatoa Huduma ya maegesho pasikuwa na risiti.
Alisema endapo mtoa huduma atabainika anatoa huduma ya maegesho pasipokuwa narisiti pamoja na Efd mtoa huduma hiyo atafikishwa katika vyombo vya sheria nakufutiwa leseni yausajili.
'' sasa tunazo mashine za kutosha zipatazo 875 za efd kwahiyo tunawaomba wanachi kuweza kudai risiti mara wanapotumia huduma yamaegesho zilizoidhinishwa na TRA ''Aliongeza Isaya mwita
No comments:
Post a Comment