Pichani
kulia ni mrembo wa Taifa Miss Tanzania
2016 Diana Edward akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara
baada ya kuwasili leo (21 Desemba 2016) akitokea Washington
DC Marekani, ambapo alikwenda kushindana katika mashindano ya urembo ya
Dunia. Miss World Beauty Contest 2016.
Miss Tanzania 2016 Diana Edward aliwasili nchini muda wa saa 10 alasiri
na Shirika la ndege la Emirates, na kulakiwa na Waandishi wa Habari,
Wazazi wake, baba na mama mzazi, wadau, pamoja na wajumbe wa Kamati ya
Miss Tanzania.
Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited utatoa ratiba ya
shughuli zake za kijamii hapo baadae, baada ya mapumziko ya mwisho wa
mwaka.
Tunawatakia Heri na Baraka za Sikukuu ya X Mass pamoja na Mwaka mpya wa 2017.
Mrembo wa Taifa Miss Tanzania
2016 Diana Edward akilakiwa na wazazi wake mara
baada ya kuwasili leo (21 Desemba 2016) akitokea Washington
DC Marekani, ambapo alikwenda kushindana katika mashindano ya urembo ya
Dunia. Miss World Beauty Contest 2016
No comments:
Post a Comment