Hapa ni katika ukumbi wa mikutano hotel ya Empire mjini Shinyanga
ambapo leo Jumatano Desemba 21,2016 waandishi wa habari mkoani Shinyanga
wamepewa mafunzo kuhusu masuala ya watu wenye ualbino.
Mafunzo
hayo yameandaliwa na Chama cha watu wenye Ualbino nchini (TAS) kupitia
programu ya Elimu kwa Jamii kuhusu mambo ya Ualbino 'Community Awareness
Raising Program' inayofadhiliwa na shirika la Open Society Foundations.
Mgeni
rasmi Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga George Mdoe aliyemwakilisha
kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akifungua semina hiyo ambapo alisema
hivi sasa serikali inahitaji watu wenye ualbino wajumuike katika jamii
ndiyo maana baadhi yao wameondolewa katika kambi zao mfano Buhangija
katika manispaa ya Shinyanga na kurudishwa katika jamii yao ili kuondoa
tofauti yao na watu wengine katika jamii.
Mwezeshaji katika
semina hiyo Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu mchango wa vyombo wa
habari katika vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino nchini
Tanzania. Malunde alisema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa
sana katika kuongeza ufahamu wa jamii juu ya masuala ya watu wenye
ualbino kitaifa na kimataifa,kupunguza matukio ya ukataji viungo vya
watu wenye ualbino na mauaji, kuelezea juhudi mbalimbali za TAS kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali.
Afisa
Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania
Josephat Torner akisikiliza hoja kutoka kwa mwandishi wa habari gazeti
la Jamboleo Stephen Kidoyayi.
..
Wednesday, 21 December 2016
Habari
No comments:
Post a Comment