Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo baada ya kukagua mitambo itakayotumika kwa huduma hiyo ambayo itaongeza ushindani wa biashara kwenye huduma za simu nchini mkoani Dodoma.
“Lazima mjipange kwenye idara ya masoko kwa kuanza kutangaza huduma hiyo kupitia njia zote zikiwemo mitandao ya kijamii, ili wananchi warahisishiwe huduma za fedha kupitia TTCL”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha, ameiagiza kampuni hiyo kupitia idara ya masoko kujipanga kuona fursa zilizopo kwa kufahamu mahitaji ya wateja wao na kuhakikisha inaongeza wateja katika mkoa huo ili kuteka soko la ushindani ambapo Serikali inajipanga kuhamia huko.
Mhandisi
wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Paul Magembe akitoa maelezo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, kuhusu
mitambo ya kutolea huduma za kifedha iliyopo katika ofisi za Kampuni
hiyo mkoani Dodoma.
Waziri Prof.Mbarawa ametaja baadhi ya
maeneo ambayo TTCL inahitaji kuboresha zaidi ni upande wa Simu (Voice)
na Data (video) ili kuweza kurahisisha mawasiliano kwa njia ya video
conference kwa kuwa kuna baadhi ya watendaji wengine watabaki Dar es
salaam.“Mkiimarisha mawasiliano upande wa data mtarahisisha hata maamuzi na pia kazi zitaenda vizuri Serikalini hasa ukizingatia baadhi ya watumishi watakuwa hapa Dodoma na wengine Dar es Salaam”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Sambamba na hilo, Waziri Mbarawa ameliagiza Shirika la Posta nchini kuja na mkakati wa kuandaa matangazo ya kutambulisha huduma ya Posta mlangoni kwa jamii ili kuiwezesha huduma hiyo kutambulika kirahisi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa
ufafanuzi kwa baadhi ya watendaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),
alipokuwa akikagua mitambo ya kutolea huduma za kifedha iliyopo katika
ofisi za Kampuni hiyo mkoani Dodoma.
Amesisitiza kwa Taasisi hizo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ili kufikia malengo waliojiwekea na kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Akiwa mkoani humo Prof. Mbarawa
amemhakikishia Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana kuboresha miundombinu
nchini hususan katika mkoa huo ikiwemo kuboresha usafiri wa anga katika
uwanja wa ndege wa Dodoma ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kuruka na
kutua.Amesisitiza kwa Taasisi hizo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ili kufikia malengo waliojiwekea na kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ameongea na watendaji pamoja na wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake na kusisitiza kufanya kazi kwa kasi, uadilifu, ubunifu na kushirikiana katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Shirika la Posta Nchini, kanda ya Dodoma Bw.
Laurent Thobias (kulia), kuhusu utoaji wa matangazo ya huduma ya Posta
mlangoni katika ofisi za Shirika hilo mkoani humo.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi
hao Meneja wa Wakala wa Majengo(TBA) mkoani humo, Arch. Masalu Bururu,
amemuahidi Waziri huyo kutekeleza yale yote aliyowà agiza ili kuleta
ufanisi na tija kwa Taifa.Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku kumi katika mikoa ya Mwanza, Mara, Arusha, Manyara na Dodoma ambapo ametembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Wizara hiyo.
Meneja
wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Mkoa wa Dodoma, Eng.
Bikulamchi Liberatus, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, kuhusu mikakati ya utengenezaji wa
magari katika karakana iliyopo Mkoani humo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza
na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo (hawapo pichani),
alipokutana nao Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment