• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 23 December 2016

    MKURUGENZI WA KIGAMBONI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA



    Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Stephen Katemba akiambatana na Meya wa Manispaa hiyo Maabad Hoja wamefanya ziara kutembelea maeneo ya uwekezaji yanayomilikiwa na Manispaa hiyo.

    Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo nikuyatambua maeneo hayo ya uwekezaji ili wafanye miradi ya maendeleo na kuiongezea mapato Halmashauri hiyo.

    Amefafanua kuwa kwa upande wa wilaya yaTemeke wananyumba mbili huku wilaya ya Kinondoni maeneo ya Haile Selasi wanaeneo la kilomita za mraba 5000 jambo ambalo litakuwa na tija kwa maendeleo ya Kigamboni, na kuongeza kuwa katika kutambua maeneo eneo la Geza Ulole ndiyo watajenga Manispaa hiyo.

    Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo Maabad Hoja ameeleza kuwa watajitahidi kusimamia maeneo hayo kikamilifu kwa kufanya uwekezaji Mkubwa, huku Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Elimu na Afya Chichi Masanja amesisitiza kuwa watajitahidi kutafuta wawekezaji kwa nguvu zote ili wilaya ya Kigamboni iwe mfano wa kuigwa kwa maendeleo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI