• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 14 December 2016

    MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATIMIZA AHADI ALIO AHIDI KWENYE ZIARA YA DAR MPYA

    Mkuu wa  mkoa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhi vifaa  mbalimbali pamoja na Fedha Taslim  ikiwa ni miongoni mwa ahadi alizozitoa wakati wakipindi cha ziara yake ya Dar mpya ambapo alikutana na malalamiko  mbalimbali kwa wananchi wa mkoa huo.
    Akikabidhi zawadi hizo Makonda amesema  ameona nivema kutimiza ahadi zake kabla kufunga mwaka  kwa yale yote aliyoyaahidi ambayo yapo ndani  ya uwezo wake.

    Pia Makonda ametoa zawadi kwa watendaji ambao waliokuwa wakionyesha umahiri wao wa kujibu na kupangua tuhuma zilizokuwa zikitolewa na wananchi  na kusema kuwa ameona niveme kuwapongeza kwa kazi kubwa walizo kuwa wakizifanya.

    Katika hatua hiyohiyo  Makonda amekabidhi mabati kwa uongozi wa shule ya secondary Jitegemee ambayo ikiwa moja ya jitihada za kuunga mkono ujenzi na ukarabati wa shule hiyo.

    Kwa upande kamanda wa fild force kanda maalumu ya Dar es salaam Stanley kabiki ametoa shukuru mkuu wa mkoa  huyo kupatiwa msaada wa gari la kubebea wagonjwa ambalo lilikuwa ni changamoto kubwa kwa upande wao kwa kipindi kirefu.

    1 comment:

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI