..
Wednesday, 28 December 2016
Habari
Akizungunza na waandishi wa habari kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa sasa Ally Salum Hapi amesema kiasi cha shilingi milioni mia sita themanini na saba, laki tisa thelathini na moja elfu na senti arobaini na nne ulikuwa umefichwa, hivyo baada ya kubaini madudu hayo wamefuatilia kwa karibu na waliwapa siku 7 kampuni hiyo ilikuweza kulipa deni hilo kwa Manispaa ya Kinondoni.
Baada ya kupata fedha hizo Manispaa imeamua kuzipeleka moja kwa moja katika ujenzi wa madarasa ya Wilaya hiyo ambapo kuna upungufu wa Madarasa 79 kwa mahesabu ya fedha hizo yatapatikana madarasa 40 yaliyokamili. Lakini pia kuna uwezekano wa kujenga shule mpya hivyo watafanya hesabu zilizo kamili ili waone kipi kinafaa.
Created By Sora Templates
Created By Bongotech
No comments:
Post a Comment