Kwa washindi MO Entrepreneurs kila mmoja amepewa mkopo wa milioni kumi ambayo ataijeresha bila kuwa na riba na kila mwanafunzi akilipiwa ada, gharama ya masomo, chakula, na malazi.
Akizungumza katika halfa ya kuwakabidhi zawadi washindi hao, Mwanzilishi wa Taasisi ya MO Dewji , Mohammed Dewji amesema ameanzisha shindano la MO Entrepreneurs ili kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili nao waweze kufanikiwa katika biashara ambazo wanafanya.
MO Dewji amesema hiyo ni sehemu ya ahadi ambayo aliitoa ya kutumia nusu ya utajiri wake kusadia watu wenye uhitaji katika jamii na nia yake ni kuona maisha ya Watanzania wenzake yanabadilika na kuwa bora zaidi kwa kuwawezesha kiuchumi kupitia ujasiriamali na elimu.
“Nilisema nusu ya utajiri wangu nitagawa kwa jamii, iwe ni afya, elimu au kwa jamii, nimeanza na nimeanza na MO Entrepreneurs, nimeanza kuwasaidia wajasiriamali 10 kupitia MO Entrepreneurs na huko mbele ninataka kuwasaidia hata wajasiriamali 10,000,” alisema MO Dewji
No comments:
Post a Comment