Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
amepokea nyumba ishirini kwa ajili ya watumishi wa afya katika wilaya za
Magu na Ukerewe mkoani Mwanza, zilizojengwa na taasisi ya Benjamin
Mkapa.
Nyumba hizo ni miongoni mwa nyumba 480
zinazojengwa na taasisi hiyo katika halmashauri 51 nchini tangu mwaka
2011, kupitia ufadhiri wa mfuko wa dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua
Kikuu pamoja na Malaria wa Global Fund.
Akizungumza kwenye hafla ya kupokea nyumba
hizo iliyofanyika katika Kijiji cha Sese wilayani Magu, Waziri Mwalimu,
amesema serikali itaendelea kuboresha nyumba za watumishi wa afya nchini
hususani wanaofanya kazi maeneo ya Vijijini.
“Nyumba hizi ni kwa ajili ya watumishi wa
afya, hatutavumilia kuona anakaa mtu ambaye siyo mtumishi wa sekta hiyo.
Tunataka kuvutia watumishi wa afya kwenda vijijini ikiwemo mwaka huu
ambapo pia tunataka tuwe na nyumba za vyumba vitatu ili mtumishi ambaye
hajaoa apate vyumba yenye vyumba viwili na aliyeoa apate nyumba yenye
vyumba vitatu”. Amesisitiza Mwalimu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini
Mkapa, Dkt.Hellen Senkoro, amebainisha kwamba nyumba hizo zimegharibu
zaidi ya shilingi Bilioni moja ambapo kila nyumba yenye baraza, sebule,
vyumba vitatu vya kulala, jiko, uzio, mfumo wa kuvuna maji wenye tenki
la lita 3,000, choo, bafu pamoja na mfumo wa umeme imegharimu wastani wa
shilingi Milioni 51. Nyumba hizo zimejengwa na Kampuni ya Grinda
Builders & Supplies.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo, amesema huduma za afya
zimeendelea kuboreshwa mkoani Mwanza ambapo kuna vituo vya kutoa huduma
za afya 388 ambapo Zahanati ni 301, Vituo vya afya 53 na Hospitali 17
na kwamba halimashauri zote zinaendelea kuhamasishwa ili kuendelea
kuongeza idadi ya vituo vya afya ili kufikia lengo la kuwa na Zahanati
kila Kijiji, Kituo cha afya kila Kata na Hospitali kila Wilaya.
Kwa mjibu wa Mganga Mkuu mkoani Mwanza,
Dkt.Leonald Subi, mkoa wa Mwanza una nyumba za watumishi wa afya
zipatazo 347 ambapo bado kuna upungufu wa nyumba 661 ili kusaidia
watumishi wa sekta hiyo kuishi karibu na vituo vyao vya kazi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akikata utepe
kuashiria upokeaji wa nyumba 20 mkoani Mwanza, zilizojengwa na Taasisi
ya Benjamini Mkapa.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
(kushoto), akimpongeza mmoja wa wauguzi wa afya katika Zahanati ya
Kijiji cha Sese wilayani Magu baada ya kupata nyumba ya kuishi ikiwa ni
miongoni mwa nyumba 20 zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
akisalimiana na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza, alipowasili katika
Kijiji cha Sese wilayani Magu kupokea nyumba 20 zilizojengwa na taasisi
ya Benjamin Mkapa.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
akisalimiana na baadhi ya watumishi wa taasisi ya Benjamin Mkapa
alipowasili katika Kijiji cha Sese wilayani Magu kupokea nyumba 20
zilizojengwa na taasisi hiyo mkoani Mwanza hii leo.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
akizungumza wakati wa halfa ya kupokea nyumba 20 zilizojengwa na taasisi
ya Benjamin Mkapa, mkoani Mwanza.
Mkuu wa
Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza wakati wa halfa ya kupokea nyumba 20 zilizojengwa na taasisi ya
Benjamin Mkapa, mkoani Mwanza.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dkt.Hellen Senkoro,
akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi nyumba 20 kwa Waziri wa Afya,
zilizojengwa na taasisi hiyo mkoani Mwanza.
Baadhi ya watumishi wa taasisi ya Benjamin Mkapa wakijitambulisha kwenye halfa hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dkt.Hellen Senkoro
(kushoto), akimkabidhi Waziri wa Afya, taarifa kuhusiana na ujenzi wa
nyumba 20 za watumishi wa wizara hiyo zilizojengwa na taasisi ya
Benjamin Mkapa mkoani Mwanza.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo akiwemo mgeni rasmi, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, wakisaini vitabu vya wageni.
Diwani wa
Kata ya Bujashi kilipo Kijiji cha Sese ambacho Zahanati yake imenufaika
na nyumba hizo, akitoa shukurani zake kwa serikali.
Mbunge wa
Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga, akizungumza katika hafla hiyo ambapo
lisha ya kuishukuru Wizara ya Afya kwa kwa kuendelea kuboresha huduma
za afya. Amemuomba Waziri wa Afya kumsaidia upatikanaji wa gari la
wagonjwa (Ambulance) katika vituo vya afya Kisesa na Ndagalu.
Baadhi
ya wakazi wa Kijiji cha Sese wilayani Magu waliohudhuria halfa ya
kupokea nyumba 20 zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa, mkoani
Mwanza.
Wapiga ngoza za asili kutoka Bujora wakitumbuizwa kwenye halfa hiyo
Wachezaji
wa ngoza za asili kutoka Bujora wakitumbuizwa kwenye halfa hiyo ya
kukabidhi nyumba 20 mkoani Mwanza, kwa waziri wa afya.
Waziri
wa afya (wa tatu kushoto) pamoja na viongozi wengine wakicheza ngoma ya
Kisukuma kutoka kwa akina mama wa Kijiji cha Sese wilayani Magu
Viongozi
mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi la kupokea
nyumba 20 za watumishi wa afya, zilizojengwa na taasisi ya Benjamin
Mkapa mkoani Mwanza
Miongoni mwa nyumba 20 za watumishi wa afya, zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani Mwanza
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Benjamin Mkapa (wawili kushoto), wakitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanahabari
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa
tatu kulia), akiteta jambo na Mganga mkuu mkoani Mwanza, Dkt.Leonald
Subi (wa nne kulia), katika Kijiji cha Sese wilayani Magu, ilipofanyika
hafla ya upokeaji wa nyumba 20 zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa
mkoani Mwanza.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
amepokea nyumba ishirini kwa ajili ya watumishi wa afya katika wilaya za
Magu na Ukerewe mkoani Mwanza, zilizojengwa na taasisi ya Benjamin
Mkapa
No comments:
Post a Comment