Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya DHAHIRI A. KIDAVASHARI DCP akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya DHAHIRI A. KIDAVASHARI DCP akionyesha vitu
mbalimbali pamoja na bunduki zilizokamatwa katika msako huo..
Bunduki na vifaa mbalimbali vinayotumika kufanyia uhalifu mkoani Mbeya vilivyoonyeshwa kwa waandishi wa habari.
Jeshi la
Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria
zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na
limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada
hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa
ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Hata hivyo
msako wa pamoja ulifanyika Wilaya ya Rungwe na kufanikiwa kukamata
silaha:-
Mnamo
tarehe 19.12.2016 majira ya saa 19:45 jioni huko Kijiji cha Busisya,
Kata ya Kisiba, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi wa
Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Askari Polisi Wilaya ya Rungwe kwa
pamoja walipata taarifa za siri za kuwepo kwa majambazi wenye silaha
ambao walikuwa na lengo la kufanya uvamizi katika Duka la Mfanyabiashara
wa soda na bia za jumla ambaye pia ni wakala wa M-Pesa ambaye
alifahamika kwa jina moja la MWANDAPILE.
Baada ya
taarifa hiyo kupatikana Askari Polisi wa Mbeya na wale wa Wilaya ya
Rungwe walianza kuwafuatilia majambazi hao na muda wa saa 19:45 jioni
huko katika barabara ya Tukuyu – Mbambo, askari walikutana na majambazi
hao wakiwa wamepakiana katika pikipiki aina ya T- Better ambayo haina
namba ya usajili yenye rangi nyekundu na baada ya majambazi hao kugundua
kuwa wanafuatiliwa na askari walianza kuwarushia risasi askari na ndipo
yalitokea majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi hao. Askari
walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili ambao walifariki papo hapo
na mmoja wao aliweza kutupa silaha aliyokuwa akiitumia na kukimbia.
Aidha
katika tukio hilo silaha bunduki tatu pamoja na risasi tisa ziliweza
kupatikana zilizokuwa zinatumiwa na majambazi hayo. Silaha hizo ni Mark
IV yenye namba 38482 na risasi mbili, Shirt Gun Greener yenye namba
G.73878 na risasi 01 na Gobole lililotengenezwa kienyeji ambalo halina
namba na risasi 06.
Aidha
baada ya kupekuliwa majambazi hao walikutwa na vitu vingine ambavyo ni
Rungu moja, Praizi moja, Bisibisi moja, mafuta ya cherehani, koti la
ngozi rangi ya brown pamoja na begi dogo rangi nyeusi ambalo lilitumika
kuhifadhi vitu hivyo.
Miili ya
marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Serikali Makandana Wilaya ya
Rungwe kwa uchunguzi wa kitabibu na bado haijatambulika. Msako
unaendelea. Katika tukio hilo hakuna mali iliyoporwa wala askari kupata
madhara. Jitihada za kumtafuta jambazi aliyekimbia zinaendelea,
Upelelezi unaendelea.
MAFANIKIO YA MSAKO NA DORIA.
Mnamo
tarehe 21.12.2016 majira ya saa 02:45 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya kwa kushirikiana na Askari wa Wanyama pori TANAPA walifanya msako
wa pamoja huko maeneo ya shule ya msingi Sangambi, Kata ya Sangambi,
Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa
kumkamata mtu mmoja aitwaye NICODEMAS S/O PIUS @ NGONYANI [57] mkazi wa
Peramiho Songea Mkoa wa Ruvuma akiwa na meno mawili ya tembo yenye uzito
wa kilogram 61 na urefu wa sentimita 150 kila moja.
Aidha
katika msako huo watuhumiwa wengine wawili wanaofahamika kwa sura
walikimbia na kutelekeza pikipiki mbili zenye namba za usajili MC 466
ASU na T.285 CHP zote aina ya shaneray rangi nyekundu walizokuwa
wamebebea nyara hizo. upelelezi unaendelea pamoja na msako mkali wa
kuwasaka watuhumiwa waliokimbia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI
anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani
havina nafasi katika jamii hii na badala yake wafanye kazi halali kwa
ajili ya kujipatia kipata halali. Pia anatoa rai kwa vijana kuachana na
tamaa za kupata mali kwa njia zisizo halali.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.(P
No comments:
Post a Comment