Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib,akizungumza na Kamati maalum itakayokutana kila muda ili kuhakikisha mradi wa kupeleka maji Hospitali ya Chake Chake unafanikiwa.
Kamati itakayosimamia mradi wa upelekaji maji Hospitali ya Chake Chake Pemba, inayoundwa na Mamlaka ya Maji ZAWA Pemba, Mawasiliano, Sheha , na Wizara ya Afya wakiwa katika kikao cha pamoja katika ukumbi wa
mikutano Hospitali ya Chake Chake.
Msimamizi wa mradi huo , Abdalla Mohammed Mbarouk, kutoka ZOP,akitowa maelezo kwa kamati ya usimamizi wa mradi wa kupeleka maji Hospitali ya chake chake -Pemba.
Mkuu wa Idara ya Ufundi ZAWA Pemba, Ali Othman, akitowa maelezo juu ya Kisima ambacho kitatumika kupeleka maji moja kwa moja kutoka Madungu hadi Hospitali ya Chake Chake-Pemba.
Daktari dhamana wa Hospitali ya Chake Chake Pemba, Ali Habib Ali,akitowa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk Khatib, juu ya maji yanavyoingia kutoka Kisima wanachotumia sasa na kuingia ndani ya Tangi la maji lilioko ndani ya Hospitali ya Chake Chake.
Mkuu wa Idara ya Ufundi wa ZAWA Pemba, Ali Othman, akifahamisha juu ya matumizi ya Kisima hicho kilichoko Madungu Chake Chake Pemba, ambacho kinatarajiwa kupeleka maji katika Hospitali ya Chake Chake Pemba.
Abdalla Mohammed Mbarouk, akionesha ramani ya mpango wa usambazaji wa maji katika Hospitali ya Chake Chake -Pemba,utakavyokuwa..
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib, akimkabidhi Kisima kinachotarajiwa kupeleka maji katika Hospitali ya Chake Chake makandarasi wa mradi huo Abdalla Mohammed Mbarouk kutoka ZOP Pemba, tayari kwa kuanza kazi .
No comments:
Post a Comment