Ushairi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ambayo imelenga kuibua vipaji vya watunga mashairi, kuuenzi mchango wa Meya wa kwanza barani Afrika ambaye pia alikuwa mshairi Abeid Amiri Kaluta, pamoja na kuitumia sanaa hiyo kujadili changamoto na maendeleo ya jiji hilo.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa shindano hilo, Chata Michael amesema mshindi wa tunzo hiyo atatangazwa kesho.
"Licha ya shindano hilo kuibua vipaji, pia limelenga kuikuza taaluma hiyo sambamba na wanataaluma wake kujitambua na kuitumia sanaa hiyo kuienzi lugha ya kiswahili," amesema.
Amesema washairi watakaofanya vizuri watarumiwa kutengeneza vitabu vya ushairi vitakavyotumika katika shule za hapa nchini.
Amesema waliojitokeza kushiriki katika shindano hilo wako 30, na kwamba mshindi wa kwanza atapata zawadi ya fedha taslimu laki tano, wa pili laki 3 wakati mshindi wa tatu ataondoka na zawadi ya laki 2.
" Mashindano hayo yatakuwa ni ya muendelezo, na mambo yakiwa vizuri hapo baadae yatahusisha mikoa yote," amesema

No comments:
Post a Comment