
WANAFUNZI 558 wa Chuo Cha kodi wametunukiwa vyeti vyao leo hii katika hii katika maafali ya tisa ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika mahafali hayo ya tisa katika hicho chuo cha kodi Dkt,Oswad Mashindano kwa niaba ya Waziri wa fedha na Mipango amesema kuwepo kwa Chuo hiki cha kodi kinatoa fursa kwa wananchi kujifunza masuala mbalimbali ya kodi na hivyo kuongeza ufahamu wao kuhusu kodi na kuwawezesha kulipa kodi bida kushurutisha.

Mashindano ametoa rai kwa menejimenti ya mamlaka ya mapato pamoja na chuo cha kodi kuitangaza kozi ya mafunzo ya forodha na usimamizi wa kodi katika nchi nyengine wanachama ili waje wajiunge kwani kwakufanya hivyo Tanzania itakuwa kinara wa mafunzo na kupata wataalamu watakao saidia Taifa kukusanya mapato.

Pamoja na hayo Mkuu wa chuo cha kodi Charse Kichere amesema miongoni mwachangamoto zinazo wakabili wanafunzi wengi wa chuo hicho wanashidwa kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa ada na fursa ya kupata mikopo.

Aidha mkuu huyo wa chuo amewapongeza wahitimu walioweza kumaliza masomo yao na amewataka kuwamabalozi wazuri katika jaamii kwa kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa ulipaji wa kodi.
No comments:
Post a Comment