• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 23 December 2016

    NDOA YA UPEPO YAFUNGWA TENA JIJINI MBEYA


    Bwanaharusi Ndugu Samwel Makalobo akivishwa pete ya ndoa na Mke wake Given Mgaya katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya .Picha na Keneth Ngelesi . 
     JamiiMojaBlog,Mbeya

    HATIMAYE lile tukio lililovuta hisia za watu wengi la bibi
    harusi, Given Mgaya, kukimbiwa kanisani na mchumba wake siku ya harusi,
    limepatiwa jibu baada ya bwana harusi , Samwel Mwakalobo, kujirudi na kuamua
    kutimiza ahadi yake ya kufunga ndoa.


    Ndoa hiyo imefungwa leo  majira ya saa tisa Desemba 23  katika Kanisa la (K.K.K.T)
    Usharika wa Isanga na kufungishwa na Mchungaji, Mathias Andangile Mwakijungu,
    huku tukio hilo likishuhudiwa na idadi kubwa ya waumini na wananchi wa kawaida
    waliojitokeza kanisani hapo.



     Kabla ya
    maharusi hao kula kiapo cha ndoa,Mchungaji Mwaijungu alitumia zaidi ya
    saa moja kutoa nasaha kwa maharusi kutokana na tukio lilotokea awali Disemba 16
    mwaka huu baada ya Bwana harusi kuingia mitini bila kutoa sababu zozote.

    Bwanaharusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23  mwaka huu.

    Bibi harusi
    akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias
    Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23  mwaka huu.


    Mbali na kutoa nasaha kwa maharusi,pia Mchungaji Mwaijungu alitumia
    fursa hiyo kuwaonya baadhi ya waumini na watu wengine kuacha tabia ya kueleza
    mambo yasiyo yajua tena bila kuwa na uhakika.


    Alisema tabia hiyo huenda ndiyo iliyosababisha tukio la
    kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo baada ya baadhi waumini na watu wengine kwa
    maslai yao walimua kueleza uzushi ulio iibua taaruki kubwa.


    Baada ya nasaha hizo na kunukukuu baadkitakatifu cha Bihi ya
    maandiko kutoka kitabu Biblia ndipo ulipo fika muda kwa maharusi hao kutimiza
    ahadi ya kula kiapo cha uaminifu katika ndoa yao

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI