Habari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda amemuapisha Kisari Matiku Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya
hivi karibuni.
Akimuapisha Mkuu huyo wa
Wilaya RC Makonda ameeleza kuwa wananchi wa Ubungo wanamatumaini na
uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha wilaya ya Ubungo ni kusogeza
huduma za wananchi karibu hivyo inabidi ahakikishe anatatua changamoto
zao kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti anazoletewa
ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji hivyo
inabidi hajiridhishe kwanza.
Katika hatua nyingine RC
Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya wote kutoruhusu wananchi kubomolewa
nyumba zao mpaka kuwepo hukumu halali ya mahakama kwani wananchi
wamekuwa wanaonewa na kudhulumiwa haki zao, hivyo wakuu wa wilaya kwa
kushirikiana na jeshi la polisi wahakikishe haki inatendeka kwa
kufuatilia ukweli na kujiridhisha kwa kuzikagua nyaraka husika.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya huyo Makori ameomba ushirikiano kwa viongozi wenzake ili aweze
kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi kuwa atafanya siasa za
kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na rasilimali zilizopo
No comments:
Post a Comment