..

Saturday, 31 December 2016
Habari
DC Mjema ameyasema hayo alipokuwa akihamasisha suala la kufanya usafi kwa vitendo ikiwa ni agizo la Rais Magufuli kwa watanzania kufanya usafi kila Jumamosi ya kila mwisho mwezi ambapo amewasisitizia kuwa suala la usafi nila kila mmoja hivyo wajitokeze kufanya usafi kwa hiari yao bila kulazimishwa kwa ilivyokuwa hapo awali.
Katika hatua nyingine DC Mjema amewataka wakazi hao kusherekea sikukuu ya mwaka mpya kwa amani bila kuchoma matairi wakiwa majumbani mwao, kwani kutakuwa na oparesheni maalum kwa watakaofanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake Naibu Meya na Diwani wa Kata hiyo Omary Kumbilamoto amewataka wakazi hao kuendelea kujitokeza kwenye usafi kama walivyofanya leo mbele ya DC Mjema kwani ni kwa faida yao wenyewe, pia Naibu Meya huyo amemkabidhi DC Mjema mbuzi kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya mwaka mpaya wa 2017 na kuunga mkono jitihada zake za kuleta maendeleo katika wilaya ya Ilala.
No comments:
Post a Comment