• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 1 January 2017

    MAKAMBA AKAGUA MIRADI YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amefanyia ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika miradi inayofadhiliwa na Ofisi yake.
    Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua mazingiza manispa ya ilala eneo la buguruni sheri 
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa kwenye ziara ya kukagua mazingira katiak maeneo ya manispa ya temeke

    Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua mazingiza manispa ya kigamboni 
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa kwenye ziara ya kukagua mazingira katiak maeneo ya manispa ya ya ilala eneo la hospital ya gakhan
    kamba-6
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amefanyia ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika miradi inayofadhiliwa na Ofisi yake.
    Akiwa katika Wilaya ya Ilala, Waziri Makamba ametembelea ujenzi wa Mfereji wa kupitishia maji taka katika eneo la Ilala Bungoni na kuongea na wananchi wa eneo hilo.
    Waziri Makamba ameugiza uongozi wa Dezo  Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.
    “Nataka mradi huu uwe wa mfano kwa ubora na viwango vya hali ya juu, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, kwa kuweka mfumo mzuri wa kukusanya maji taka na kuyaelekeza sehemu stahiki” Makamba alisisitiza.
    Aidha, Waziri Makamba amewataka wakazi wanaozuka eneo hilo kuacha mara moja utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa, na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela kutoa adhabu kali kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.
    “Kwa kupitia kamati za Mazingira za vitongoji na sheria ndogo ndogo mlizojiwekea hakikisheni kuwa hifadhi ya mazingira inazingatiwa kwa mstakabali wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.”
    Pia, Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha Wakandarasi wanaopewa kazi za ukusanyaji wa taka, wanakuwa na vifaa na uwezo wa kutosha kwa kuhakikisha taka zote zinazolewa kwa wakati ili kuepuka mrundikano wa taka katika makazi ya watu.
    “Natoa wito pia kwa vijana wa maeneo haya kuunda vikundi vidogo vya kuzoa taka ili kuwa chanzo cha ajira kwenu.” Makamba alisisitiza.
    Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira –  NEMC kutembelea eneo hilo la Ilala Bungoni na kutoa maelekezo kwa Gereji bubu  zinazokiuka hifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa kufanya shughuli zao pembezoni mwa mfereji unaojengwa.
    Ujenzi wa Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Aidha, Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya kazi ya ujenzi huu na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.
    Waziri Makamba katika ziara yake hii leo ametembelea Ilala Bungoni, Mtoni kwa Azizi Ali, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kutembelea eneo la Ujenzi wa Ukuta Barabara ya Obama.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI