Katika taarifa yao waliitoa mapema leo kupitia mtandao wa WhatsApp wa Wanahabari Tanzania (WANAHABARI TZ) ilieleza: “Azimio lililopitishwa na waandishi wote wa Arusha ni kwamba Mwandishi yoyote atakayeenda kufanya ‘coverage’ ya Lukuvi Leo atatengwa. Tunaombwa kuungana USA River kituo cha Polisi kushinikiza mwenzetu Halfan atolewe mahabusu.” Ilieleza taarifa hiyo.
Hata hivyo taarifa za awali zilieleza kuwa mwandishi huyo alitakiwa kupelekwa Mahakamani ambapo kupitia wanahabari wa mkoa huo, Wakili aliyewekwa na THRDc alipoenda kuongea na Khalfan Liundi, OCSID akakataza Wakili kuongea na Mteja wake lakini baadae OCSID alikanusha juu ya kosa la Uchochezi na kuelezwa kuwa yupo ndani kwa oda ya Mkuu wa wilaya.
Mpaka sasa Wanahabari kwa umoja wao bado wapo katika kituo hicho cha Polisi kusubiria hatima ya mwanahabari huyo, Mo blog itaendelea kukupatia kila kinachoendelea huko.
Unaweza kusoma zaidi tukio hili: http://bit.ly/2i4cPaL
Na Mwandishi Wetu Arusha
Mwandishi Khalifan Liundi
No comments:
Post a Comment