Habari
Wafanyakazi wa Kamati ya Maafa Zanzibar
na ile ya sherehe na mapambo,wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia
maadili ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa.
Akizungumza na wafanyakazi hao katika ofisi ya kamati hiyo Forodhani
mjini Zanzibar, Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Mihayo Juma Nhunga amewataka kuvumilia mazingra magumu yanayowakabili
katika utendaji wao.
Nhunga amesema, kwa kuwa dunia
inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira, hivyo waliopata nafasi
hiyo waiheshimu kwa kuwajibika ipasavyo
na kwa mujibu wa kanuni na miongozo ya kazi sambamba na kuwasisitiza
watendaji hao kuepuka kujenga matabaka sehemu za kazi, akisema kufanya hivyo kunarejesha nyuma harakati za kuleta maendeleo.
Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati
ya Maafa Ali Juma Hamad, amesema wanakabiliwa na changamoto ya uelewa
mdogo walionao wananchi kuhusiana na maafa sanjari na ukosefu wa elimu,
wananchi hushindwa kufuata taratibu zinazopaswa wakati kunapotokea
maafa nchini au katika baadhi ya maeneo.
Wafanyakazi wa idara hizo wamelalamikia uhaba wa vitendea kazi ikiwemo
usafiri na kompyuta, ambapo wamesema hali hiyo inawapa usumbufu mkubwa
sambamba na kuiomba serikali, kuangalia kwa uzito mkubwa maslahi ya
wafanyakazi ingawa imekuwa ikijitahidi kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
No comments:
Post a Comment