Habari
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Tabora,
kimewasimamisha kazi kwa muda usiojulikana Mwenyekiti chama hicho wilaya
ya Igunga,Joseph Kashindye na Katibu wake, Idd Athuman.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani hapa Katibu wa Chadema
Mkoa wa Tabora, Ally Mwakilima alisema viongozi hao wamesimamishwa
uongozi tangu Novemba 30, mwaka huu baada ya kukiuka katiba ya chama
hicho.
Alisema kuwa uamuzi ya kuwasimamisha yametolewa na baraza la uongozi
la mkoa kupitia chama hicho baada ya viongozi hao wawili kukiuka na
kuvunja katiba ya chama ibara ya 10:3(4)(maadili ya wanachama).
Katibu huyo alisema tarehe Novemba 28 mwaka huu, viongozi hao wawili
walisimama mbele ya mahakama ya wilaya iliyopo mjini Tabora kutoa
ushahidi upande wa mtu aliyeshitaki chama huku wakiwa wanajua wazi kuwa
ni kinyume na katibu ya chama ibara ya 10:3 kifungu cha (4) maadili ya
wanachama.
Aidha katibu huyo alibainisha kuwa pamoja na kuwasimamisha viongozi
hao, pia baraza la chama hicho limemuagiza katibu wa wilaya wa chama
hicho, Idd Athuman kukabidhi mali zote za chama kwa katibu wa jimbo la
Igunga mbele ya mwenyekiti wake ikiwa ni pamoja na kujieleza ndani ya
siku 14.
Athumani na Kashindye wamekiri kupokea barua ya kusimamishwa tangu Desemba 3, mwaka huu yenye kumbukumbu namba CDM/M/TBR/WG/01.
Hata hivyo, Athumani alisema yeye haoni kosa lolote kwa kuwa aliitwa
na mahakama kwenda kutoa ushahidi wa mwanachama aliyekwenda mahakamani
kutafuta haki ambayo hakupewa na chama.
“Kama kuitwa mahakamani kutoa ushahidi kuwa ni kosa basi katibu wa
mkoa hana kosa kunisimamisha uongozi lakini kama si kosa kusimamishwa
uongozi kumetoka wapi? alihoji katibu.
Sambamba na hayo katibu huyo alibainisha kuwa yeye ataendelea kuwa
mwanachama kwa kuwa chama chake bado anakipenda na hatasita kutoa
ushirikiano wakati wowote atakapohitajika.
Kwa upande wao baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao hawakutaka
majina yao kuandikwa katika gazeti, wamesema viongozi wa mkoa na wilaya
wanapaswa kukaa meza moja kwa kuwa viongozi wao Athumani na Kashindye
hawaoni kosa walilofanya kwani wao waliitwa na mahakama
No comments:
Post a Comment