| Mkurugenzi wa taasisi ya ECONNRCT Hashim Magesa wa kwanza kushoto akizungumza na wanahabari |
Tafiti zilizotolewa na bank kuu ya dunia kupitia delivery indicators imeonyesha kuwa 37% ya waalimu waliokutwa mashuleni hawakuwa madarasani katika muda wa masomo hali inayopelekea kushuka kwa viwango vya elimu nchini
Amesema hayo leo mkurugenzi mtendaji wa ECONNECT Bwn Hashimu Magesa alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam leo,ambapo amesema kuwa jambo hilo la kukosekana kwa waalimu madarasani katika muda wa masomo linaashiria kuwa wanafunzi hawapati elimu kwa kiwango kilichokusudiwa na wizara ya elimu na mamlaka yake
Bwn Magesa amesema kutokana na utafiti wa majaribio walioufanya kwenye wilaya ya ilala kwa jumla ya shule 152 ampo katika zoezi hilo waliorodhesha taarifa mbalimbali za kielimu kupitia takwimu sahihi ambazo kwa sasa zinawapa taarifa na kuokoa fedha ambazo zingetumika kuchapisha taarifa na huku taarifa hizo zikifika kwa haraka kwa wahusika
Hta hivyo taasisi ya ECONNECT imetoa wito kwa serikali kuutumia mfumo wa majaribio kwa ndani ya mwaka mmoja ili kujiridhisha na ufanisi wake,pia taasisi inawataka wadau mbali mbali wa elimu ikiwa ni pamoja na makampuni,taasisi na watu binafsi kushirikiana kwa pamoja kwaajili ya kuwezesha utekelezaji wa mfumo utakaosadia kuboresha elimu hapa nchini kwa manufaa ya taifa letu kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment